Nani Anaweza Kuomba Huduma za AIC?

1. Kampuni, ushirika au mtu binafsi ambaye amepita awamu ya uanzishaji wa kilimo biashara na anaweza kuonesha uwezekano wa biashara kukua.

2. Wahitimu wa vyuo na vijana wengine wenye mawazo bunifu ya kilimo biashara watachaguliwa kujiunga na kituo cha kutamia vijana (Incubation Center). 

3. Makampuni au wamiliki wa kilimo biashara yenye matatizo na zinazoyumba au kueleka kufungwa sokoni kutokana na sababu mbalimbali. 

4. Wanawake wajasiriamali kwenye kilimo biashara watapewa kipaumbele.

Sifa za Kuomba Kupatiwa Huduma za AIC

1. Awe amefanya kilimo biashara angalau kwa muda wa mwaka au zaidi

2. Awe na taarifa za biashara kuonesha mapato na matumizi ya miaka iliyopita

3. Kwa vijana watakao jiunga na vituo vya kutamia wawe na wazo bunifu au uzoefu wa kilimo biashara 

4. Kampuni zenye matatizo ya uendeshaji baishara (madeni, uongozi dhaifu, ushindani)

5. Wanawake wajasiriamali kwenye kilimo biashara watapewa kipaumbele

 

 

 

Go to top