Kupakua fomu hili, bonyeza: FOMU YA MAOMBI KITUO ATAMIZI CHA SUA-AIC, MOROGOROKITUO ATAMIZI CHA KILIMOBIASHARA,

SUA AIC, MOROGORO

 

TANGAZO KWA VIJANA

Kituo cha Ubunifu wa Kilimobiashara (AIC), idara ya Taasisi ya PASS inapenda kutangazia kwamba inapokea maombi ya vijana ya kujiunga na Kituo Atamizi cha Kilimobiashara SUA-AIC, Morogoro.

Katika kituo hiki, AIC inawapa fursa vijana wenye ueledi wa ujasiriamali, maarifa na uzoefu katika kilimo na wenye kiwango chochote cha elimu kote nchini, kuanzisha, kumiliki na kuendesha biashara.

Kijana atakayeomba nafasi hii anatakiwa awe na tabia njema, mtiifu, mwenye  nidhamu, mchapa kazi, fikra chanya, mwaminifu na anayependa kuona matokeo chanya.

Vijana wa kike watapewa kipaumbele.

Vijana washiriki kwenye Kituo Atamizi watapewa vifaa, miundo mbinu, malighafi na mtaji wa kufanya kilimobiashara ambapo watausimamia kwa kipindi cha miezi 12.

Katika kipindi chote, waatamiwa watapewa usimamizi wa karibu ikiwemo ushauri wa kibiashara na upelembaji, ili kuhakikisha wanafanikiwa katika shughuli zao za kilimobiashara. Baada ya kukamilika kwa muda huo, vijana watakaofanikiwa kwenye kilimobiashara, AIC itawawezesha kufanikisha kuanzisha biashara kama hiyo kwenye eneo lao.

Vijana wenye nia wanashauriwa kutuma maombi yao ya kujiunga na Kituo Atamizi cha SUA-AIC. Vijana 200 watachaguliwa kwenye awamu ya kwanza ya mchujo na kati ya hawa, kwenye awamu ya pili ya mchujo, vijana 70 watachaguliwa kujiunga na Kituo Atamizi kuanzia Oktoba 2019.

Maelezo zaidi na fomu ya maombi yanapatikana kwenye tovuti ya www.aic.co.tz na www.pass.or.tz, ofisi za SUA/SAEBS na ofisi zote za PASS nchini.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 12/08/2019.

 

 

Go to top