Oktoba 2018:

Kituo Atamizi cha Kilimobiashara, Morogoro, kimeanza kuatamia vijana 20 kwenye kilimobiashara cha mbogamboga kwa kutumia shambanyumba (screenhouse). Vijana hawa watamaliza kipindi chao cha uatamizi baada ya miezi 12, yaani Septemba 2019.

 

Julai 2019:

Kituo Atamizi cha Kilimobiashara, Kongwa, kimeanza kuatamia vijana 10 kwenye unenepeshaji wa mbuzi. Vijana hawa watamaliza kipindi chao cha uatamizi mwezi wa Juni 2020.

 

Julai 2019:

Maombi mapya ya kujiunga na Kituo Atamizi, Morogoro, yametangazwa. Vijana 200 watachaguliwa kwenye awamu ya kwanza ya mchujo na kati ya hawa, kwenye awamu ya pili ya mchujo, vijana 70 watachaguliwa kujiunga na Kituo Atamizi kuanzia Oktoba 2019.

 

Mengineyo:

Mipango ya kuanzisha vituo atamizi kwenye maeneo mengine nchini na kwenye shughuli mbalimbali kama ufugaji wa samaki, ng’ombe wa maziwa, na usindikaji na uzalishaji wa bidhaa (agroprocessing) yanaendelea.

Go to top