Kutamia Vijana kwenye kilimobiashara
AIC inawatamia vijana katika vituo vyake atamizi vya kilimobiashara (Youth Agribusiness Incubators) kwa ajili ya kuwawezesha kuwa wajasiriamali kwenye sekta ya kilimo, hasa kwenye usindikaji na uzalishaji wa bidhaa zitokanazo na mazao ya kilimo.
Vituo Atamizi hivi vipo kwenye sekta mbalimbali ya kilimo kama mbogamboga (kwa kutumia shambanyumba na umwagiliaji wa tonetone), kilimo cha wazi (open field), ufugaji (mbuzi, ng’ombe wa maziwa, kuku, sungura, n.k.), uvuvi (samaki ya kufuga kwenye matanki na vizimba), usindikaji na uzalishaji wa bidhaa zitokanazo na kilimo.
Kwa sasa, vituo viwili vilivyopo Morogoro na Kongwa vimeshaanza kuatamia vijana. Vituo vingine vinakusudiwa kufunguliwa Dodoma, Zanzibar, Dar es Salaam, Tanga, Kanda ya Ziwa, na Kanda ya Juu Kusini.
AIC inashirikiana na taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa za elimu, utafiti na kilimobiashara kufanikisha shughuli hii ya kutamia vijana. Taasisi hizo zikiwemo Sokoine University of Agriculture (SUA), Tanzania Livestock Research Institute (TALIRI), Small and Medium Industry Development Agency Zanzibar (SMIDA), Tanzania Agriculture Development Bank (TADB), International Crops Research Institute for the Semi-Arid Tropics (ICRISAT), na mengineyo.
AIC inazingatia kwa makini sana maswala ya vijana, jinsia na mazingira. Kwenye shughuli zake zote, kipaumbele kinatolewa kwa vijana, wanawake na utaratibu wa uzalishaji uliorafiki kwa mazingira.