Usimamizi wa Masoko
• Utafiti wa Soko (uridhishwaji wa mteja, maendeleo ya bidhaa na huduma, idadi ya watu, umri, kipato na elimu ya wateja, nk.)
• Mpango Mkakati wa Soko (utambuzi wa dhamira, uchambuzi wa hali, malengo ya masoko, mkakati na tathmini, na B4: Bango-Bidhaa-Banda-Bei)
• Uuzaji & Usambazaji (lengo la mauzo, mkakati wa mauzo na usambazaji, mbinu/mpango kazi)
Usimamizi wa Fedha
• Mifumo ya Uhasibu (kuchagua njia ya uhasibu, njia ya kurekodi mihamala, chati ya mpangilio wa vitabu vya hesabu, matumizi ya mifumo ya hesabu, uoanishaji wa taarifa za hesabu za biashara na za benki)
• Uwekaji Hesabu (ushauri juu ya matumizi ya double entry bookkeping, kuchambua akaunti ya leja, taarifa za mauzo na gharama, stoku, taarifa za mapato, mizania)
• Usimamizi wa Mtiririko wa Fedha (cash flow)
Usimamizi wa Uendeshaji
• Malighafi (upatikanaji, wauzaji, usafirishaji, bei)
• Uzalishaji/Uchakataji (mikakati ya mchakato wa uzalishaji, mikakati ya uwezo)
• Bidhaa (uendelezaji, uzalishaji, umuhimu kwa wateja, gharama, athari kwa bidhaa nyingine, upekee, na ubora)
• Uhifadhi (uwezo wa ghala, muda wa uhifadhi, udhibiti na uangalizi wa stoku, uingizaji na utoaji bidhaa na malighafi)
• Ufikishaji wa Bidhaa (usafirishaji, makubaliano na mawakala)
• Gharama na Ufanisi (ushauri wa namna ya kupunguza gharama na uboreshaji wa ufanisi)
Usimamizi wa Rasilimali Watu
• Ueledi & Uhitaji wa Wafanyakazi (kuajiri, kuelekeza, motisha, kuunda timu ya uuzaji, upimaji wa uwezo na sifa za mfanyakazi)
• Mchanganuo wa Shughuli na Usimamizi wa Wafanyakazi
Teknolojia & Usimamizi wa Ubunifu
• Uendelezaji wa Bidhaa (vivutio vya bidhaa kwa wateja, ubunifu na undaji wa bidhaa mpya, majaribio ya bidhaa mpya)
• Teknolojia (inayofaa, inakopatikana, ugavi, ufungaji mashine, uhakiki wa ufanisi wa mashine)
• Uendeshaji & Matengenezo (kuwaunganisha na watalaamu wa mashine)
Ushauri wa Mahitaji ya Udhibiti
BRELA, TRA, OSHA, WCF, NSSF, TFDA, TBS, NEMC, LGAs, WMA, nk.
Mitandao ya Biashara
Uvumishaji wa biashara, vyama vya biashara, kushiriki kwenye maonesho, nk.