Nani Anaweza Kuomba Huduma za AIC?
• Kampuni, ushirika au mtu binafsi ambaye amepita awamu ya uanzishaji wa kilimo biashara na anaweza kuonesha uwezekano wa biashara kukua.
• Wahitimu wa vyuo na vijana wengine wenye mawazo bunifu ya kilimo biashara wanaochaguliwa kujiunga na kituo cha kutamia vijana (Incubation Center).
• Makampuni au wamiliki wa kilimo biashara yenye matatizo na zinazoyumba au kueleka kufungwa sokoni kutokana na sababu mbalimbali.
• Wanawake wajasiriamali kwenye kilimo biashara.
Sifa za Kuomba Kupatiwa Huduma za AIC
• Awe amefanya kilimo biashara angalau kwa muda wa mwaka au zaidi.
• Awe na taarifa za biashara kuonesha mapato na matumizi ya miaka iliyopita.
• Kwa vijana watakao jiunga na vituo vya kutamia wawe na wazo bunifu au uzoefu wa kilimo biashara.
• Kampuni zenye matatizo ya uendeshaji baishara (madeni, uongozi dhaifu, ushindani).
• Wanawake wajasiriamali kwenye kilimo biashara watapewa kipaumbele.