Sisi ni Nani?
Kituo cha Ubunifu wa Kilimo Biashara (AIC) ni idara ndani ya Taasisi ya PASS inayolenga kutoa huduma za maendeleleo ya biashara kwa wajasiriamali wa kilimo biashara wenye mrengo wa kukua kibiashara. Aidha, AIC inatoa kipaumbele kwa kilimo biashara zinazowahusisha au kumilikiwa na vijana na wanawake.
Lengo la AIC:
Kusaidia ukuaji wa kilimo biashara kwa kuongeza ufanisi na tija ili kukuza ushindani katika masoko ya ndani, kikanda na kimataifa. Hili litafikiwa kwa kuwapatia wajasiriamali waanzilishi maarifa ya Kilimo biashara, kuwaunganisha na mitandao ya biashara, teknolojia, masoko na upatikanaji wa mitaji/fedha zinazohitajika kukuza biashara zao.
Dira Yetu:
Kuwezesha wajasiriamali wa kilimo biashara wakiwemo vijana na wanawake kukuza biashara zao zaidi.
Dhamira Yetu:
Kutoa huduma za kitaalamu na maalum za maendeleo ya biashara kwa wakulima wa kilimo cha kisasa na wasindikaji wa mazao ya kilimo ili waweze kupanua biashara zao zaidi.
Faida kwa Wajasiriamali
AIC huwasadia wajasiriamali kukuza biashara zao - kwa faida zaidi!
Inawapatia wajasiriamali mbinu za mpango bora wa kilimo biashara, kuboresha mifumo ya utunzaji wa kumbukumbu, usimamizi wa masoko na fedha, na kuboresha ufanisi kwenye mchakato wa usindikaji na ugavi wa malighafi. Pia, mjasiriamali hufaidika kwa kupewa maarifa ya kufikiri kimkakati zaidi, kuboresha teknolojia, kupunguza gharama za biashara, na kupanga mipango ya fedha. Vilevile, kuunganishwa na mabenki kwa ajili ya mitaji/fedha, wauzaji wa malighafi, wasambazaji wa bidhaa na watoa huduma za maendeleo ya biashara.